Wednesday, June 20, 2012

OMOTOLA kuizindua Super Star ya Wema Jumapili Giraffe HotelNi katika onyesho maalum la familia
MKALI wa filamu nchini Nigeria na Afrika, Omotola Jalade

atazindua filamu ya Wema Sepetu Jumapili hii katika Ukumbi

wa Hoteli ya Girafee Ocean View, iliyopo Mbezi Beach.
Filamu hiyo iitwayo Super Star imechezwa na Wema,

ikionyesha maisha ya mtu maarufu na changamoto

anazozipata ikiwemo kuandikwa mambo mbalimbali ikiwemo

taarifa za vyombo vya habari.
Katika uzinduzi huo, bendi kutoka Tanzania House Of Talent

(THT) watatoa burudani, kabla ya mashabiki kupata nafasi ya

kupiga picha na msanii huyo.
Omotola, ambaye ni mke wa rubani Kapteni Matthew

Ekeinde, ambao walifunga ndoa yao angani kwenye ndege

atatoa nafasi ya kupiga picha na watu kadhaa.
Katika uzinduzi huo, pamoja na burudani ya muziki,

mashabiki watakaofika hapo, watapata pia fursa ya kuiona

filamu ya Super Star katika viwanja hivyo vya hoteli hiyo

iliyoko ufukweni.
Omotola ambaye yuko kwenye ndoa kwa miaka 16 akiwa na

watoto wanne, ana jumla ya albamu mbili za muziki.Msanii

huyo ambaye mwaka jana alitangaza kuachana na kucheza

filamu kutokana na kuandikwa vibaya, anatarajiwa kuwa

kivutio kikubwa kwenye uzinduzi huo ambao kiingilio kitakuwa

Sh 30, 000 kwa wakubwa na watoto 10,000.

No comments:

Post a Comment